CLASSIC INFORMER TZ

Thursday, 25 August 2016

Leo katika historia Alhamisi tarehe 25/08/2016


Miaka 149 iliyopita katika siku kama hii ya leo alifariki dunia msomi mashuhuri wa Uingereza Michael Faraday.  Faraday alizaliwa mwaka 1791 mjini London na licha ya kuwa hakuwa na elimu ya juu lakini alifanikiwa kupata maendeleo muhimu katika fizikia na kemia kwa kutumia majaribio na tajiriba.  Tarehe 24 Novemba miaka 184 iliyopita, Michael Faraday aligundua chombo cha mkondo wa umeme kinachojulikana kwa kitaamu kama ''Electric Current''. Kwa ugunduzi huo Faraday akawa amefanikiwa kupiga hatua kubwa katika elimu ya fizikia. Miongoni mwa mafanikio mengine makubwa yaliyoletwa na mtaalamu huyo ni ugunduzi wa mota ya umeme pamoja na kubadilisha nguvu za sumaku kuwa nguvu za umeme.

Katika siku kama ya leo miaka 921 iliyopita sawa tarehe 25 Agosti mwaka 1095, vilianza Vita vya Msalaba kati ya Wakristo na Waislamu.Katika vita hivyo wafuasi wa kanisa walichora alama za msalaba kwenye mabega na mavazi yao, na kwa sababu hiyo vita hivyo vimekuwa maarufu kwa jina la Vita vya Msalaba. Baada ya vita vingi na Waislamu, wapiganaji wa msalaba hatimaye waliuteka na kuukalia kwa mabavu mji wa Baitul Muqaddas huko Palestina mnamo mwaka 1099.Mji huo ulikombolewa mwaka 1187 na wapiganaji wa Kiislamu waliokuwa wakiongozwa na Salahuddin Ayyubi

Na siku kama ya leo miaka 28 iliyopita Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitoa azimio nambari 620 likilaani hatua ya Iraq ya kutumia silaha za kemikali.

No comments:

Post a Comment