Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa ameandika barua kuhusu
operesheni ya chama chake iliyopewa jina la Ukuta na jinsi ambavyo jeshi
la Polisi na Serikali lilivyopanga ‘kuubomoa’.
Katika
waraka huo, Lowassa ameeleza kuwa ameamua kushika kalamu na kuandika
masikitiko yake kuhusu hali ya amani nchini akidai Serikali imekata
mkono wa amani.
Ameeleza kuwa Serikali imekandamiza upinzani na demokrasia na ndio chanzo cha wao kuanzisha UKUTA kupinga ukandamizaji huo.
“Binafsi
nafurahishwa na kutiwa moyo na jinsi watanzania walivyoipokea
Operesheni hii, pamoja na vitisho vya dola,” ameandika. “Siku zote sisi
Chadema na Ukawa kwa ujumla ni wenye kulitakia amani na utulivu Taifa
letu. Maandamano haya ya Septemba 1 ni ya amani, lakini vitendo vya
jeshi la polisi vimewapa wasiwasi Watanzania,” Lowassa ameongeza.
Katika
andiko hilo, Lowassa amedai kuwa amekuwa akipigiwa simu na viongozi
wastaafu pamoja na watu mashuhuri wakimshauri kushawishi wakae na
Serikali kuzungumza ili kuepusha taifa kujiingiza katika machafuko.
Aliongeza kuwa kukutana na Rais John Magufuli katika Jubilee ya miaka 50
ya ndoa ya Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa ni sehemu ya juhudi hizo.
“Nyote
ni mashahidi wa tukio la kukutana na Rais Magufuli katika Jubilei ya
miaka 50 ya ndoa ya mzee Mkapa. Ulikuwa ni mwanzo wa juhudi zetu za
kuwanyooshea mkono wa amani. Lakini tunashangazwa wenzetu hawako tayari
kuupokea mkono huo,” ameandika.
Aliongeza
kuwa katika kikao cha juzi cha ndani cha chama hicho kilichofanyika
katika Hotel ya Giraffe jijini Dar es Salaam walipanga kuzungumzia jinsi
ya kuunyosha zaidi mkono wa amani lakini Jeshi la Polisi ‘liliukata’.
No comments:
Post a Comment