CLASSIC INFORMER TZ

Thursday, 1 September 2016

Je wajua kufungua baadhi ya tovuti unaweza ibiwa data zako zote za siri kwenye simu au laptop

Kuna mamilioni ya tovuti zisizo salama na kwa kuzifungua tovuti hizo tu huweza kusababisha kuibiwa datazako za siri nyingi kutoka kwenye kifaa chako kiwe ni simu au Laptop, jifunze jinsi ya kujikinga.

Huduma ya mtandao imeleta mafanikio makubwa sana kwenye jamii ila isipotumika kwa uangalifu inamadhara makubwa sana kwa jamii. Kuna hatua kadhaa unaweza chukua ili kuzuia data zako za siri kutoibiwa hatua hizo ni:-

  1. Tumia vifungua tovuti salama na vinavyoenda na wakati marazote kama Mozilla na Google Chrome ila pia hakikisha marazote unafatilia update kutoka kwa mtengenezaji wa program yako unayotumia kufungulia tovuti na program nyinginezo.
  2. Usihifadhi kumbu kumbu za siri kwenye vifunguzi hivyo,marakadhaa watu wamekuwa wakiona uvivu kuingiza password zao mara kwa mara na kuomba vifunguzi hivyo kukumbuka password zao nihatari sana kwa usalama wa data zako, hakikisha password yako huiifadhi popote zaidi ya kuikumbuka kichwani.
  3. Hakikisha unatumia Antivirus ya kulipia na si za bure ili upate kibali cha kuhakikishiwa usalama zaidi.
  4. hakikisha untivirus yako ipo updated mudawote wa matumizi.
  5. Hakikisha computer Firewall ipo wazi muda wote kukukinga na wavamizi wanaoingia kwenye kifaa chako bila ya wewe kujua unapo kuwa kwenye internet.

Lowassa Aandika Waraka Mzito Kuhusu Oparesheni UKUTA


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa ameandika barua kuhusu operesheni ya chama chake iliyopewa jina la Ukuta na jinsi ambavyo jeshi la Polisi na Serikali lilivyopanga ‘kuubomoa’.
 
Katika waraka huo, Lowassa ameeleza kuwa ameamua kushika kalamu na kuandika masikitiko yake kuhusu hali ya amani nchini akidai Serikali imekata mkono wa amani.
 
Ameeleza kuwa Serikali imekandamiza upinzani na demokrasia na ndio chanzo cha wao kuanzisha UKUTA kupinga ukandamizaji huo.
 
“Binafsi nafurahishwa na kutiwa moyo na jinsi watanzania walivyoipokea Operesheni hii, pamoja na vitisho vya dola,” ameandika. “Siku zote sisi Chadema na Ukawa kwa ujumla ni wenye kulitakia amani na utulivu Taifa letu. Maandamano haya ya Septemba 1 ni ya amani, lakini vitendo vya jeshi la polisi vimewapa wasiwasi Watanzania,” Lowassa ameongeza.
 
Katika andiko hilo, Lowassa amedai kuwa amekuwa akipigiwa simu na viongozi wastaafu pamoja na watu mashuhuri wakimshauri kushawishi wakae na Serikali kuzungumza ili kuepusha taifa kujiingiza katika machafuko. Aliongeza kuwa kukutana na Rais John Magufuli katika Jubilee ya miaka 50 ya ndoa ya Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa ni sehemu ya juhudi hizo.
 
“Nyote ni mashahidi wa tukio la kukutana na Rais Magufuli katika Jubilei ya miaka 50 ya ndoa ya mzee Mkapa. Ulikuwa ni mwanzo wa juhudi zetu za kuwanyooshea mkono wa amani. Lakini tunashangazwa wenzetu hawako tayari kuupokea mkono huo,” ameandika.
 
Aliongeza kuwa katika kikao cha juzi cha ndani cha chama hicho kilichofanyika katika Hotel ya Giraffe jijini Dar es Salaam walipanga kuzungumzia jinsi ya kuunyosha zaidi mkono wa amani lakini Jeshi la Polisi ‘liliukata’.
 
“Kitendo kile kwangu binafsi kimezidi kuniimarisha na kunipa nguvu zaidi ya kudai demokrasia na kuheshimu katiba ambayo viongozi wetu waliapa kuifuata na kuitetea,” unasomeka waraka wa Waziri Mkuu wa zamani, Lowassa.