Kampuni ya simu za samsung yakubali yaishe
Kampuni
ya kutengeneza simu za smartphone ya Samsung imeamua kusitisha
utengenezwaji wa simu aina ya Samsung galaxy note 7 ambayo siku za hivi
karibuni imeonekana kuleta kizaazaa miongoni mwa watumiaji wake.
Taarifa
kutoka kwa maafisa wa juu wa kampuni hiyo ambao hata hivyo hawakutaka
majina yao yajulikane, zimedai kampuni hiyo itasitisha utengenezaji wa
simu za aina hiyo huku ikiendelea kuzifanyia uchunguzi kuhusu matatizo
yaliyomo.
Hali
hii inakuja baada ya kampuni mbili nchini Marekani kuzuia uuzwaji wa
simu hizo. Itakumbukwa kampuni hiyo ilitangaza kuzifanyia mabadiliko
simu za Note 7 za awali na baada ya kujiridhisha ilizipeleka sokoni tena
ingawa zilizobadilishwa nazo zimeonekana kuleta matatizo.
Matukio
ya hivi karibuni ya kuungua kwa aina ya simu hizo kwenye ndege na kuzua
tafrani miongoni mwa abiria huenda ndio yaliyopelekea kampuni hiyo
kufikiria upya kuhusu simu hizo.
No comments:
Post a Comment