Bodi ya ligi Tanzania imethibitisha timu
za Simba na Yanga zitautumia uwanja wa Uhuru kwa mechi zao za nyumbani
baada ya serikali kuzizuia kuutumia uwanja wa taifa kama uwanja wao wa
nyumbani kwenye mechi zao za ligi kuu.
Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Boniface
Wambura amesema, mechi ijayo ya Yanga wataanza kucheza kwenye uwanja huo
dhidi ya Mtibwa mchezo unaotarajiwa kuchezwa Alhamisi October 13.
“Mechi zao watacheza kwenye uwanja wa
Uhuru, kwahiyo mechi zao zote za nyumbani watakuwa wakitumia uwanja huo.
Serikali ilizifungia kutumia uwanja wa taifa, uwanja wa Uhuru uko wazi
wanaweza kuutumia wakati wowote,” anathibitisha Boniface Wambura.
Awali vilabu hivyo vilikuwa vinautumia
uwanja huo kwa mechi zao za ligi kabla ya Simba kuulamimikia kuwa
unawasababishia majeraha wachezaji wao na kuomba kurudishwa kwenye
uwanja wa taifa.
Serikali ilichukua uamuzi wa kuufungia
uwanja wa taifa kufatia vurugu za mashabiki zilizozuka kabla na wakati
wa mchezo wa Yanga vs Simba uliochezwa October Mosi. Kabla ya mechi
hiyo, mashabiki waling’oa mageti manne kabla ya mashabiki wa Simba
kung’oa viti wakati mechi ikiendelea kwa madai klabu yao ilikuwa
ikionewa katika mchezo huo.
No comments:
Post a Comment