Siku kama ya leo miaka 156 iliyopita, Paul Gottlieb Nipkow mmoja wa wavumbuzi wa televisheni alizaliwa huko Ujerumani. Nipkow alikulia katika familia maskini, lakini juhudi yake thabiti aliyokuwa nayo ilimuwezesha kuendelea na masomo yake ya fizikia hadi akafika Chuo Kikuu. Paul Gottlieb Nipkow alifanya utafiti mkubwa na hatimaye alifanikiwa kuvumbua transimita ya televisheni. Chombo hicho kilichobuniwa na Nipkow kilikuwa na uwezo wa kurusha mawimbi ya televisheni hadi umbali wa mita 30 tu na baadaye transimita iliyotengenezwa na mvumbuzi huyo wa Kijerumani ilikamilishwa na wabunifu wengine
Miaka 339 iliyopita katika siku kama ya
leo, vilijiri vita vya mwisho vya La Rochelle kati ya Wakatoliki na
Waprotestanti wa Ufaransa. Vita hivyo vilianza baada ya Waprotestanti
kuchochewa na Uingereza. Wakatoliki ambao walikuwa wakiungwa mkono na
vikosi vya jeshi la serikali ya Ufaransa chini ya uongozi wa Richelieu,
Kansela mashuhuri wa nchi hiyo, walipigana vita na Waprotestanti ambao
walikuwa wakipigania maeneo yao katika bandari ya La Rochelle. Vita
hivyo vilimalizika baada ya mwaka mmoja kwa kupata ushindi Wakatoliki na
kukaliwa kwa mabavu La Rochelle.
Katika siku kama ya leo miaka 318
iliyopita, mkataba wa pande tatu wa Russia, Poland na Denmark ulitiwa
saini dhidi ya Sweden. Wafalme wa nchi hizo tatu walikuwa na lengo la
kumuangusha Sharel XII mfalme kijana wa Sweden ili kuikalia kwa mabavu
nchi hiyo. Ni kwa msingi huo ndipo miaka miwili baadaye mnamo mwezi
Aprili mwaka 1700 nchi wanachama wa mkataba huo wa pande tatu zikaamua
kuishambulia Sweden, hata hivyo jeshi la mfalme Sharel XII likakabiliana
vilivyo na kutoa pigo kwa nchi vamizi. Baada ya kufikia mapatano na
Denmark, mwaka 1704 akaishambulia Poland na kuikalia kwa mabau. Hata
hivyo mashambulio ya Sharel dhidi ya Russia hayakuzaa matunda.
No comments:
Post a Comment