Utafiti unaonyesha kuwa madaktari wa
nchi za kusini mwa Afrika wanatoa dawa nyingi zaidi ya zilizoagizwa na
Shirika la Afya Duniani WHO.
Utafiti huo uliofanywa na Chuo kikuu cha
London kwa ushirikiano na kituo cha Kutoa ushauri wa afya cha nchini
Ghana,ikihusisha nchi kumi na moja za kusini mwa jangwa la Sahara
zinaonyesha kuwa wagonjwa wanapewa takribani dawa tatu kila
wanapotembelea hospitali, moja zaidi ya maelekezo ya WHO.
Inasemekana tatizo ni baya zaidi kwenye taasisi zinazotengeneza faida, na kuchochea kuuza dawa.
Tafiti zimeonya kuwa matumizi makubwa ya
madawa yanasababishwa na kulazimishwa kutumia dawa, kuzidisha dozi na
kuleta athari mbaya kwa mchanganyiko unaosababishwa na kuchanganya dawa
mbalimbali.
Pia wamegundua wagonjwa wengi wamekuwa
wakipewa dawa za kutuliza maumivu pasipo kufanyiwa vipimo, na kuongeza
hatari ya maambukizo yanayosababisha na kupambana na dawa.
No comments:
Post a Comment