Ikiwa
zimesalia siku tatu kufika tarehe 14 ambayo ni kumbukumbu ya kifo cha
baba wa Taifa mwalimu Julius Nyerere, Leo October 11 2016 BBC
wameripoti taarifa ya Chancellor wa Ujerumani Angela Merkel kuzindua
jumba jipya la makao makuu ya Umoja wa Afrika ambalo limepewa jina la
baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Jumba hilo ambalo jina lake kamili ni Jumba la Amani na Usalama la Julius Nyerere
limejengwa kwa ufadhili kutoka Ujerumani, litakuwa makao ya idara ya
Amani na Usalama ya AU na litatumiwa pia na maafisa wa kutoa tahadhari
ya mapema kuhusu mizozo barani pamoja na kuratibu juhudi za kulinda
amani za AU.
Ujenzi wa
jumba hilo, ambalo ukubwa wake wa sakafu ni mita 13,500 mraba na
linaweza kutumiwa na wafanyakazi 360, uligharimu euro milioni 27. Jumba
hilo ofisi za kufanyia kazi, vyumba vya mikutano vya kutumiwa na Baraza
la Amani na Usalama, chumba cha kuratibia shughuli, maktaba na vyumba
vya shughuli za pembeni.
Mwalimu
Nyerere, ambaye alikuwa rais wa Tanzania hadi 1985, alikuwa mmoja wa
viongozi waanzilishi wa Muungano wa Nchi za Afrika (OAU) ambao sasa ni
Umoja wa Afrika (AU). Alishiriki sana katika jitihada za kuendeleza bara
la Afrika na kusaidia mataifa ambayo hayakuwa yamepata uhuru kujipatia
uhuru wake.
No comments:
Post a Comment