Kutoka
Shirika la afya duniani WHO leo October 11, 2016 mtu wangu nakuletea
taarifa hii kuhusu madhara ya matumizi ya Sukari kwenye nchi nyingi
duniani ambayo yamepelekea WHO kuzitaka serikali za nchi husika kuanza
kutoza kodi kubwa kwenye vinywaji vinavyotumia sukari, ili kupambana na
tatizo la unene uliopindukia maarufu kama Obesity, likisema kuwa kufanya
hivyo kutapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya vinywaji vya sukari.
Mapendekezo
haya ya shirika la afya duniani kuhusu vinywaji vyenye sukari, yamekuja
wakati huu dunia ikijidhatiti kupunguza tatizo la uzito uliopindukia,
ambapo kwa sasa mtu mzima mmoja kati ya watatu ana tatizo hilo.
WHO
inasema kuwa, kuna ushahidi wa kutosha kwamba utozaji wa kodi ya ziada
kwa vinywaji vinavyotumia sukari kutasababisha kupunguza tatizo na
watumiaji wa vinywaji hivyo hasa kwa kuongeza kodi kwa zaidi ya asilimia
20.
Kwa maneno
mengine, nyongeza ya asilimia 20 itapunguza matumizi ya unywaji wa
vimiminika vya sukari kwa zaidi ya asilimia 20, huku asilimia 50 ya
nyongeza ya kodi, kutapunguza karibu nusu yake, shirika hilo limesema.
Wakati huo
huo idadi ya watu wanaougua ugonjwa wa kisukari duniani imeendelea
kuongezeka tangu mwaka 1980, kutoka watu 108 hadi watu milioni 422 mwaka
2014.
Kwa mujibu
wa shirika la habaru la Reuters Ugonjwa wa uzito uliopindukia pamoja na
kisukari umesababisha vifo vya watu milioni 1 na laki tano mwaka 2012,
huku magonjwa yanayohusishwa na matumizi makubwa ya sukari na kupelekea
watu kuugua kisukari ukisababisha vifo vya watu milioni 2 na laki 2.
No comments:
Post a Comment