CLASSIC INFORMER TZ

Friday, 5 July 2019

Afrika yatafuta mwenyeji wa eneo huru la biashara kuunganisha masoko yake


Political map of Africa with capitals and major cities
RAMANI YA BARA LA AFRIKA


Viongozi wa kiafrika watafanya maamuzi siku ya Jumapili taifa gani litakuwa mwenyeji wa makao makuu ya eneo huru la biashara barani humo, ambalo litalenga hatimaye kuwaunganisha watu bilioni 1.27 barani humo na pato lao la jumla la taifa ambalo ni dola trilioni 3.4.
Viongozi katika mkutano wa Umoja wa Afrika unaofanyika Niger pia watapanga tarehe ya kuanza biashara eneo huru la biashara ambalo litajulikana kama African Continental Free Trade, matafia 52 kati ya 55 wametia saini makubaliano hayo.
Umoja huo hatimaye unataka kuondoa vikwazo vya biashara na ushuru kati ya mataifa wanachama.
Kwa mujibu wa kanuni za AU, wanachama wake wote wanaweza kuwasilisha maombi ili kuteuliwa kuwa makao makuu ya eneo huru la biashara. Kenya, Ghana, Eswatini, Madagascar na Misri wamewasilisha maombi. Ethiopia na Senegal waliamua kujitoa katika ushindani huo.
Walio katika ushindani wa sasa wamegawanyika katika kanda kuu za bara hilo: Kenya inatokea mashariki, Ghana kutoka magharibi, eSwatini kutoka kusini wa Afrika, Madagascar inawakilisha visiwa vya bahari ya Hindi na Misri inawakilisha eneo la kaskazini.
Misri ambayo pia inashikilia urais wa AU mwaka huu imekuwa ikihamasisha na kujitaja kuwa kiini katika biashara barani Afrika.
Misri ni moja ya wanachama wa siku nyingi wa Umoja wa Afrika na inafurahia uhusiano wenye nguvu na mataifa mengine ya Afrika, amesema afisa wa kutoka wizara ya biashara Misri na kuongeza kuwa wana vigezo vyote vinavyohitajika.
Kenya na Misri tayari ni wenyeji wa ofisi za taasisi za kimataifa na pia wana mashirika ya ndege yanayotajika sana barani humo.
Kenya ni mwenyeji wa makao makuu ya idara za Umoja wa Mataifa kwa mazingira na maendeleo mijini. UNEP na UN- Habitat. Misri ni mwenyeji wa makamo ya Africa Export Import Bank.
“Nairobi ni eneo la kiasili sana kwa taasisi kama hiyo. Ni rahisi kufika sehemu yoyote katika bara hilo kutoka hapa Nairobi,” Peter Munya, waziri wa biashara wa Kenya amewaambia waandishi wa habari.
Taifa dogo la eSwatini ambalo zamani lilikuwa linajulikana kama Swaziland, limepata uungaji mkono kutoka taasisi ya kieneo ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADCC).
Taifa lolote ambalo litachaguliwa kuwa mwenyeji wa makao makuu ya biashara litapata fursa ya kufungua milango ya ajira kwa raia wake na kupata msaada wa fedha kwa ajili ya sekta za usafiri na utalii.
AU inataka kuongeza biashara yake mpaka asilimia 25 – 36 kwa mwaka ndani ya bara hilo katika muda wa kipindi cha miaka mitano, kutoka asilimia 18 kiwango cha sasa, na kuvutia uwekezaji wa muda mrefu kutoka makampuni makubwa ya utengenezaji magari duniani.
Siku ya Jumapili viongozi wa AU mbali ya kuteua nchi ambayo itakuwa mwenyeji wa makao makuu ya biashra huru, pia watazindua kanuni zinazohusu masuala kama vile biashara huru, kuondolewa kwa vikwazo vya ushuru na mifumo ya malipo .
Imewasilishwa kwenu na Ditro Josia,Ngara Tanzania 

BOOMPLAY KUBORESHA TASNIA YA MUZIKI NCHINI TANZANIA





Image result for manager wa boomplay



Boomplay kuboresha tasnia ya muziki nchini Tanzania, yatangaza kushirikiana zaidi na wasanii wa Tanzania
MENEJA WA BOOMPLAY TANZANI BI NATASHA STAMBULI
Dar es Salaam Boomplay, app inayoongoza barani Afrika kwa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki, yafanya forum yake ya kwanza kwa ajili ya wasanii nchini Tanzania.
Katika forum hiyo, Meneja wa Boomplay Tanzania Bi Natasha Stambuli alizungumza kuhusu kuwezesha wasanii na uzalishaji wa muziki (Production) na usambazaji wa muziki kidigitali (Digital Distribution).
“Boomplay tunatambua changamoto mbalimbali zinazowakabili wasanii kama kupata muda wa studio, ku-shoot video zenye quality ya kimataifa na mengine mengi. Tumeingia mkataba na Wanene Entertainment ili kuwezesha wasanii na matatizo hayo.”
“Barani Afrika Boomplay ina ofisi Tanzania pamoja na Kenya, Nigeria na Ghana. Moja kati ya fursa zinazopatikana ni sisi kuwa na uwezo wa kujenga madaraja kwa wasanii wetu wa Tanzania na wasanii wengine kutoka nchi hizo” aliendelea Bi Natasha Stambuli.
Forum hiyo ilijumuisha jopo la wataalamu mbalimbali katika tasnia ya muziki akiwemo Bi Martha Huro – Meneja wa Boomplay Kenya, Lupakisyo Mwambinga – Mkuu wa Idara Ya Sheria COSOTA, Nahreel kutoka Navy Kenzo,G Nako-Weusi, Moses Range – Muanzilishi DEMO Innovators, Japhet Kapinga – Meneja Maudhui Boomplay na kuratibiwa na msanii wa miondoko ya Hip Hop, Wakazi.
Wasanii na watayarishaji pia walipata nafasi ya kuuliza maswali kwa wataalamu hao na kupata ujuzi zaidi katika masuala ya sheria, hati miliki, branding na vingine vingi katika tasnia ya muziki.
Kuhusu Boomplay
Boomplay (ambayo awali ilikuwa ikifahamika kama Boomplayer), ni jukwaa linalotoa huduma ya kusikiliza na kupakua (download) muziki ambayo ipo chini ya umiliki wa kampuni ya Transsnet Music Limited.
Malengo ya app hii ni kutengeneza jukwaa kubwa na la kutegemewa na wasanii na wazalishaji wa muziki katika usambazaji wa kazi hizo za sanaa. Kwa sasa Boomplay ndio application kubwa na inayokuwa kwa kasi sana barani Afrika, ikiwa na nyimbo na video zaidi ya milioni 5.
Watumiaji wake wanaweza kusikiliza na kuangalia video bure, kwa kujisajili (subscribe) kupitia vifurushi vya siku,wiki au vile vya mwezi ambapo ambavyo vinawawezesha kuhifadhi (save) nyimbo offline au kununua nyimbo. Huduma hiyo kwa sasa inapatikana Android, iOS na wavuti.
Mnaonaje kuhusu hili wadau?

Tuesday, 14 February 2017

ditroyosia@gmail.com


Ndugu zangu nawaombeni tembeleeni kwenye Blog yangu ili kupata habari tofauti tofauti zilizojiri na vile vile nahitaji kutunga simulizi mbalimbali ko nahitaji support yenu kwa hili  
Kwani najua bila mawazo yenu sitofanikisha hili na hata kama una story yako nzuri ya kusisimua usisite kuwasiliana nami kupitia email yangu hapo juu,Twitter @ditroyosia1,Instagram Dittolyto tz,Facebook ditto lyto tz 
kwa mawasiliano simu ya kiganjani ni;
0757634776 Vodacom
0625953090 Halotel
Nawapenda sana nyote

Tuesday, 11 October 2016

PICHA 10: Jionee list ya Top 10 ya meli za gharama zaidi Duniani

Najua kuna watu wanafuatilia vitu mbalimbali na gharama zake, naomba nikusogezee TOP 10 ya meli za gharama zaidi duniani, katika list hii namba mbili imeshikwa na meli ya Harmony of the seas ambayo ni  meli kubwa ya abiria kwa sasa duniani na imezinduliwa miezi kadhaa tu iliyopita.
Namba moja imeshikwa na meli ya Allure of the Seas na safari yake ya kwanza ilifanyika miaka sita iliyopita Allure of the Seas ndio ilikuwa meli kubwa duniani kabla ya meli ya Harmony of the seas kuwepo.

10. Norwegian Breakaway ($840 million)

.

9. Disney Dream ($900 million)

.
.

8. Norwegian Escape ($920 million)

.

7. Quantum of the Seas ($935 million)

7

6. Anthem of the Seas ($940 million)

6

5. Disney Fantasy ($950 million)

5

4. Norwegian Epic ($1.2 billion)

4

3. Oasis of the Seas ($1.3 billion)

3

2. Harmony of the Seas ($1.35 billion)

2

1. Allure of the Seas ($1.43 billion)

1

Matumizi ya Sukari kwa binadamu yamezidi kiwango, WHO wametoa agizo hili..

Kutoka Shirika la afya duniani WHO leo October 11, 2016 mtu wangu nakuletea taarifa hii kuhusu madhara ya matumizi ya Sukari kwenye nchi nyingi duniani ambayo yamepelekea WHO kuzitaka serikali za nchi husika kuanza kutoza kodi kubwa kwenye vinywaji vinavyotumia sukari, ili kupambana na tatizo la unene uliopindukia maarufu kama Obesity, likisema kuwa kufanya hivyo kutapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya vinywaji vya sukari.
http://i2.wp.com/www.aawellnessproject.org/wp-content/uploads/2016/07/1401309063000-AP-Obesity1.jpg?w=620
Mapendekezo haya ya shirika la afya duniani kuhusu vinywaji vyenye sukari, yamekuja wakati huu dunia ikijidhatiti kupunguza tatizo la uzito uliopindukia, ambapo kwa sasa mtu mzima mmoja kati ya watatu ana tatizo hilo.
WHO inasema kuwa, kuna ushahidi wa kutosha kwamba utozaji wa kodi ya ziada kwa vinywaji vinavyotumia sukari kutasababisha kupunguza tatizo na watumiaji wa vinywaji hivyo hasa kwa kuongeza kodi kwa zaidi ya asilimia 20.
Kwa maneno mengine, nyongeza ya asilimia 20 itapunguza matumizi ya unywaji wa vimiminika vya sukari kwa zaidi ya asilimia 20, huku asilimia 50 ya nyongeza ya kodi, kutapunguza karibu nusu yake, shirika hilo limesema.
Wakati huo huo idadi ya watu wanaougua ugonjwa wa kisukari duniani imeendelea kuongezeka tangu mwaka 1980, kutoka watu 108 hadi watu milioni 422 mwaka 2014.
Kwa mujibu wa shirika la habaru la Reuters Ugonjwa wa uzito uliopindukia pamoja na kisukari umesababisha vifo vya watu milioni 1 na laki tano mwaka 2012, huku magonjwa yanayohusishwa na matumizi makubwa ya sukari na kupelekea watu kuugua kisukari ukisababisha vifo vya watu milioni 2 na laki 2.

Heshima nyingine aliyopewa Mwl Nyerere Afrika

Ikiwa zimesalia  siku tatu kufika tarehe 14 ambayo ni kumbukumbu ya  kifo cha baba wa Taifa mwalimu Julius Nyerere, Leo October 11 2016 BBC wameripoti taarifa ya Chancellor  wa Ujerumani Angela Merkel kuzindua jumba jipya la makao makuu ya Umoja wa Afrika ambalo limepewa jina la baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Jumba hilo ambalo jina lake kamili ni Jumba la Amani na Usalama la Julius Nyerere limejengwa kwa ufadhili kutoka Ujerumani, litakuwa makao ya idara ya Amani na Usalama ya AU na litatumiwa pia na maafisa wa kutoa tahadhari ya mapema kuhusu mizozo barani pamoja na kuratibu juhudi za kulinda amani za AU.
Ujenzi wa jumba hilo, ambalo ukubwa wake wa sakafu ni mita 13,500 mraba na linaweza kutumiwa na wafanyakazi 360, uligharimu euro milioni 27. Jumba hilo ofisi za kufanyia kazi, vyumba vya mikutano vya kutumiwa na Baraza la Amani na Usalama, chumba cha kuratibia shughuli, maktaba na vyumba vya shughuli za pembeni.
Mwalimu Nyerere, ambaye alikuwa rais wa Tanzania hadi 1985, alikuwa mmoja wa viongozi waanzilishi wa Muungano wa Nchi za Afrika (OAU) ambao sasa ni Umoja wa Afrika (AU). Alishiriki sana katika jitihada za kuendeleza bara la Afrika na kusaidia mataifa ambayo hayakuwa yamepata uhuru kujipatia uhuru wake.

MSAMI - STEP BY STEP (OFFICIAL MUSIC VIDEO)

Barakah The Prince, Alikiba - Nisamehe [Official Video]

Stan Bakora - NISAMEHE Parody ( By Baraka The Prince X Alikiba)

Shetta aliwahi kuosha gari la star wa Bongo fleva?

Kampuni ya simu za samsung yakubali yaishe


Kampuni ya kutengeneza simu za smartphone ya Samsung imeamua kusitisha utengenezwaji wa simu aina ya Samsung galaxy note 7 ambayo siku za hivi karibuni imeonekana kuleta kizaazaa miongoni mwa watumiaji wake.

Taarifa kutoka kwa maafisa wa juu wa kampuni hiyo ambao hata hivyo hawakutaka majina yao yajulikane, zimedai kampuni hiyo itasitisha utengenezaji wa simu za aina hiyo huku ikiendelea kuzifanyia uchunguzi kuhusu matatizo yaliyomo.

SUMSUNG NOTE 7

Hali hii inakuja baada ya kampuni mbili nchini Marekani kuzuia uuzwaji wa simu hizo. Itakumbukwa kampuni hiyo ilitangaza kuzifanyia mabadiliko simu za Note 7 za awali na baada ya kujiridhisha ilizipeleka sokoni tena ingawa zilizobadilishwa nazo zimeonekana kuleta matatizo.

Matukio ya hivi karibuni ya kuungua kwa aina ya simu hizo kwenye ndege na kuzua tafrani miongoni mwa abiria huenda ndio yaliyopelekea kampuni hiyo kufikiria upya kuhusu simu hizo.

New song

(4.50MB)Download Mwasiti fEAT Lady Jaydee - WITO.mp3

2 days ago
Download nyimbo mpya ya Mwasiti fEAT Lady Jaydee - WITO.mp3