CLASSIC INFORMER TZ

Wednesday, 24 August 2016

Mwanamitindo amkabidhi Waziri Nape tuzo ya Canada

Herieth Paul
Herieth Paul
NA DITTO LYTO,
MWANAMITINDO wa   Kimataifa, Mtanzania Herieth Paul, amemkabidhi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, tuzo ya mwanamitindo bora wa mwaka (Model of the Year 2016) aliyotunukiwa na Canadian Annual Art & Fashion Awards (CAFA).
Tuzo hiyo ya mwanamitindo bora wa mwaka ya Canada huwa na ushindani mkubwa kwani hutolewa kwa mwanamitindo aliyeonyesha kiwango cha juu na aliyetoa mchango mkubwa katika tasnia hiyo nchini Canada, ambapo shindano hilo lilifanyika Aprili 14 mwaka huu.
Herieth ambaye kwa sasa anasomea biashara kwa mwaka wa pili kwa njia ya mtandao nchini Canada, aliishukuru Serikali kwa kupokea tuzo hiyo ya kwanza kwake na kwa taifa.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Waziri Nape alimpongeza mwanamitindo huyo kwa kuipeperusha vema bendera ya Tanzania na kuahidi kumsaidia anapohitaji msaada kutoka kwa Serikali.
“Serikali tunajitahidi kumsaidia kadiri ya uwezo wetu pale anapohitaji msaada, pia kama kuna vijana walikuwepo ndani na nje ya nchi wenye kipaji na kupeperusha vema bendera ya nchini, wajitokeze kwani hii ni kupanua wigo wa uchumi wa taifa pamoja na kujitangaza,” alisema Nnape.
Herieth aliipongeza Serikali kwa kukubali wito wake wa kumkabidhi tuzo hiyo aliyoipata nchini Canada kwa kuwa mwanamitindo wa kwanza, huku akiwatupa chini wanamitindo wanne kutoka katika nchi hiyo.
“Siwezi kuahidi kitu kwa Serikali kwani hii ni tuzo yangu ya kwanza, kikubwa ni kuhakikisha naendelea kuitangaza Tanzania kupitia kipaji changu hicho cha mitindo,” alisema.

No comments:

Post a Comment