Afrika ni miongoni mwa Bara lililobarikiwa tamaduni, lugha na watu tofauti wenye tabia zinazoshabihiana ikiwamo ukarimu.
Miongoni mwa watu wa Bara hili wapo
wasichana warembo wa kuvutia tofauti na wengine, katika hili kuna
mjadala mpana huku baadhi wakikubali kuwa kuna watu wanaovutia kuliko
wengine huku baadhi yao wakidai kuwa uzuri, urembo wa mtu unatafsiriwa
kulingana na anayemtizama.
Lakini katika hili tukubali tukatae
miongoni mwa wanawake wa Afrika bila kujali wanatizamwa na nani ni
wazuri na warembo na wanavutia kuliko wengine.
Ifuatayo ni orodha ya nchi 10 zenye
wanawake wenye mvuto barani Afrika, mwaka jana Tanzania ilishika nafasi
ya 10 mwaka huu imepanda nafasi moja na inashika nafasi ya tisa.
10: Ghana
Nchi ya Ghana inashika namba 10 kwa kuwa
na wanawake wazuri Barani Afrika kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa Machi
mwaka huu na tovuti mbalimbali za masuala ya urembo ikiwamo Afrojuju,
Urbanviralmedia.
Jambo wanalolingana wanawake wa Ghana kuwa wana mvuto wa asili ambao huuongezea kwa kujiremba.
Mwaka jana Ghana ilishika namba nane, mwaka huu imeshuka nafasi mbili na kushika nafasi ya 10.
9: Tanzania
Nafasi ya tisa mwaka huu imeshikiliwa na Tanzania iliyokuwa inashikilia nafasi ya 10 mwaka jana hivyo imepanda nafasi moja.
Miongoni mwa sifa za wanawake wa
Tanzania ukiachilia mbali uzuri wa asil ni ni pamoja na kutunza nyumba,
ujuzi wa kukisafisha chumba na kukipamba. Katika orodha hii wametajwa
kuwa wanawake bora wachapa kazi na wanaojali familia.
8: Kenya
Imepanda nafasi moja kwa kuwa mwaka jana ilishika nafasi ya tisa.
Sifa za wanawake wa nchi hiyo ni pamoja
na kuwa wajuzi katika mapenzi, wachapa kazi na watuamiaji wa pombe,
jambo linalowatofautisha na watu wengine ni rangi yao ya kuvutia.
7: Nigeria
Kwa miaka miwili mfululizo warembo wa Nigeria wanashikilia nafasi ya saba.
Wanawake wa Nigeria licha ya kuwa na
rangi za kuvutia, pia wana maumbo ya yaliyojazia na wamejaaliwa kuwa na
uwezo wa kuzaa watoto wengi, kati ya 1970 na 2011 Nigeria iliongezeka
idadi ya watu mara tatu na kuifanya kuwa nchi yenye wakazi wengi barani
Afrika. Kama unataka mwanamke mzuri na atakayekuzaliwa watoto wengi
Nigeria inakuhusu.
Kwa wale wanaotaka mwanamke mwenye sifa za kuwa mke, wa nchi hiyo wanafaa. Sifa ya kipekee wanajua kupika na kutunza familia.
6: Ivory Coast
Mwaka huu namba sita imeshikiliwa na
Ivory Coast ambayo mwaka jana haikuwepo kabisa, hivyo imeingia kwenye 10
bora kwa mara ya kwanza, nafasi hiyo mwaka jana ilishikwa na nchi ya
Afrika Kusini.
5: Afrika Kusini
Nchi hii imewapa jina warembo wake
“Upinde wa Mvua wa Taifa”. mwaka huu imepanda nafasi moja kutoka nafasi
ya sita iliyoshika mwaka jana.
Ni miongoni mwa nchi zenye wasichana
warembo wa kuvutia katika Bara la Afrika. Miji ya Cape Town,
Johannesburg, Pretoria na Durban ndiyo yenye wanawake wenye mvuto.
Wanawake wa Afrika Kusini wanang’aa na kuvutia kutokana na ngozi zao
nyororor.
Unapofika nchini humo hasa katika Jiji
la Pretoria kuwa makini kwa sababu unaweza kugongwa na gari kutokana na
kuwashangaa warembo hao ambao kwa kawaida huvaa tofauti kidogo, nguo zao
huwa fupi.
4: Rwanda
Wanaume wao hujivunia kwa kuwaita “Tufaa
Lililojificha”, mwaka jana nchi hiyo ilishika nafasi ya kwanza kwa kuwa
na wanawake warembo, mwaka huu imekamata nafasi ya nne.
Wanawake wa nchi hii sifa ya kipekee
ikiwamo urefu unaopendeza, shepu ya Kiafrika kabisa, wasomi na wanaotaka
kufahamu kila jambo.
Kitu kinachowafanya wawe juu licha ya
kuwa warembo, ni wachapa kazi wanaojali muda na kupigania wanachokitaka
bila kujali wanapambana na nani na ana nafasi gani ikiwamo kutoogopa
mashindano na wanaume katika nyanja mbalimbali ikiwamo za kisiasa,
kielimu au kiutendaji.
3: Somalia
Sifa yao maarufu na wanayopendwa kuitwa
na wanaume wa nchi yao ni “Vita Aiharibu Urembo”, mwaka jana walishika
nafasi ya pili. Licha ya urembo na kuwa karibu maeneo mengi katika Bara
la Afrika bado wana utamaduni wa kuoana wao kwa wao. Wanatajwa pia kuwa
miongoni mwa wanawake wanaoamini katika ndoa na kuitendea haki.
2: Eritrea
Ni miongoni mwa nchi zenye wanawake
wenye mvuto barani Afrika, licha ya asilimia kubwa ya wanawake wake
kujihifadhi kwa kuvaa ushungi na mavazi marefu bado asili ya urembo wao
ipo pale pale.
1: Ethiopia
Wanawake wa nchi hii huitwa “Asili ya Ubinadamu”. Huo ni utambulisho wao mbele ya macho ya dunia.
Inaelezwa kuwa ustaarabu kwa wanawake
ulianzia katika Ethiopia, hivyo inatajwa kuwa ni nchi yenye wanawake
wenye mvuto zaidi barani Afrika.
Wengine wanasema matokeo ya mvuto wao
yanatokana na mchanganyiko wa watu wa kale wa Yemen na Ethiopia. Wakati
mwingine inakuwa ngumu kuwatofautisha kutokana na baadhi yao kufanana
sana, maumbile, sura na uzungumzaji.