Kuna mengi sana unaweza ukawa ushasikia
sana kuhusu njia nzuri za kuchaji simu yako. Pia utakuwa umeshasikia
kuhusu ambayo hutakiwi kufanya ukiwa unachaji simu. Je yana ukweli
wowote? Leo tutakuelezea kwa uchache na kwa ukweli mambo muhimu kuhusu
kuchaji kwa simu na usalama wa betri za simu wakati tukiwa tunazichaji
1. Kutumia chaja ambazo si za makampuni ya
simu zinaua simu? Hapana, hakuna ukweli kabisa katika hili ila ukweli
ni kwamba usitumie chaja za ubora mbovu. Chaja feki si chaja zote ambazo
hazitengenezwi na kampuni husika ya simu bali ni chaja ambazo zipo
chini ya kiwango. Na hizi utazigundua kupitia bei zake, usikubali
kumiliki simu ya gharama halafu ukawa mbahili katika kununua chaja za
uhakika kisa bei zake. Cha kufanya soma kuhusu kiwango na ubora wa
chaja inayofaa kwenye simu yako kabla ya kununua chaja isiyokuja na simu
yako.
2. Usitumie simu yako wakati unaichaji?
Si kweli, ni kweli zamani sana, kwa sasa teknolojia inayotumika kwenye
chaja na simu ni salama kabisa. Cha kuhakikisha ni kwamba unatumia
chaja zilizo na kiwango/ubora wa uhakika (original/quality). Kumbuka
hapa haimaanishi ni kwamba lazima iwe ni yenye lebo/nembo ya kampuni
husika bali hili ni suala la kuwa ni chaja yenye ubora wa uhakika.
3. Usizime simu yako kamwe!? Si kweli!
Unashauliwa kuzima simu yake angalau ata mara moja kwa wiki kwa angalau
lisaa. Simu kama vifaa vingine vyote vya umeme ni muhimu kupata muda wa
kupumzishwa. Na jambo hili ndio linaboresha zaidi uhai wa simu yako.
4. Kuchaji simu usiku kucha
kutaiua/haribu? Usisikilize hii…si kweli! labda kama unatumia simu
iliyotengenezwa miaka ya 1980 :-). Teknolojia imekua sana, fahamu ya
kwamba simu zote za siku hizi zitaacha kutumia umeme pale simu yako
itakapochaji hadi asilimia 100! Itaacha kuchaji! Hakuna madhara! Ila hii
haimaanisha ndio uiache kwa zaidi ya masaa 15! na pia kuhakikisha
unaichaji sehemu inayopata hewa
5. Subiri hadi chaji iwe chini kabisa au
imeisha ndio uchaji? Hili sio kweli! Ukweli ni kwamba kuchaji mara kwa
mara ndio kunasaidia zaidi kuongeza maisha ya betri yako. Kumbuka
kuchaji mara kwa mara si kila baada ya dakika 5, bali ni kwamba
usisubiri chaji iwe chini ndio uchaji, na si lazima ukiweka kwenye chaji
usiitoe hadi imejaa.
6. Kuna aina kuu mbili za mabetri
yanatumika kwa sasa Kuna mabetri yanayotumia teknolojia ya Lithium-Ion
(Li-ion) na Lithium-Ion-Polymer (Li-ion polymer/Lithium Polymer). Kuna
teknolojia nyingi zilizokuwepo zamani ila kwa sasa hizi ndio
zinazotumika zaidi. Na zinatumika kutokana na ubora wake. Lithium-Ion
(Li-ion) zinatumika zaidi katika simu nyingi zaidi wakati mabetri ya
Lithium-Ion-Polymer yanatumika zaidi katika laptop na baadhi ya simu
pia.
Lithium-Ion-Polymer ndio teknolojia bora
zaidi na salama zaid, lithium-Ion ni salama pia kwa kiwango kikubwa sana
ila lithium-ion-polymer ni zenye ubora zaidi na hii inaweza kuwa ni
sababu kubwa zinatumika kwenye laptop nyingi tayari. Teknolojia hizi
zimefanya ulipukaji ovyo wa mabetri ya simu kuwa mgumu sana kuliko
unavyofikiri.